The House of Favourite Newspapers

Jukwaa La Women’s Network Forum La Vodacom Lajadili Nafasi Iliyonayo Kuleta Usawa Wa Huduma Za Kijiditali

0
Mkurugenzi wa Fedha Vodacom Tanzania Plc, Bi. Hilda Bujiku (mwenye kipaza sauti) akizungumza wakati wa jukwaa la Women’s Network Forum lililoandaliwa na kampuni hiyo kujadili nafasi iliyonayo katika kuleta usawa kwenye huduma za kidigitali Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Wakimsikiliza ni jopo la majaji kutoka Vodacom Tanzania Plc walioshiriki jukwaa hilo la majadiliano kulia kwake ni Athumani Mlinga, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Mawasiliano na kwenda kushoto kwake ni Mcberthana Wilfred, Meneja wa Usalama wa Mtandaoni na Teknolojia ya Mawasiliano, Niamini Yonazi, Mtengeneza Programu, na Aileen Meena ambaye alikuwa ni mwendesha mjadala.                                                                                                                                                                                               
Meneja wa Usalama wa Mtandaoni na Teknolojia ya Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, Mcberthana Wilfred (mwenye kipaza sauti) akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo (hawapo pichani) wakati wa jukwaa la Women’s Network Forum lililoandaliwa na kampuni hiyo kujadili nafasi iliyonayo katika kuleta usawa kwenye huduma za kidigitali Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Wakimsikiliza kulia ni Mkurugenzi wa Fedha Vodacom Tanzania Plc, Bi. Hilda Bujiku, na kushoto ni Niamini Yonazi, Mtengeneza Programu, na Aileen Meena ambaye alikuwa ni mwendesha mjadala.                                                                                                                                                                                                                      
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye picha ya Pamoja ikiwa ni ishara ya kukumbatia usawa wa kijinsia kwenye ubunifu na teknolojia kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Kusherehekea siku hiyo jukwaa la kampuni hiyo la Women’s Network Forum lilikutana na kujadili mada zinazohusiana na ubinifu na teknolojia katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.                                                                                                                                                                                                   
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakifuatilia kwa makini wazungumzaji wa jukwaa la Women’s Network Forum (hawapo pichani) lililoandaliwa na kampuni hiyo kujadili nafasi iliyonayo katika kuleta usawa kwenye huduma za kidigitali Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu ni ‘Ubunifu na Teknolojia kwa usawa wa kijinsia’.
Leave A Reply