The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Apigiwa Shangwe Na Chadema Kwenye Kongamano La Siku Ya Wanawake Duniani – Bawacha

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshiriki Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lilioandaliwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA ( BAWACHA) katika Ukumbi wa Kuringe – Mkoa wa Kilimanjaro Machi 08, 2023.

“Napenda kuwaambia kuwa hili ni kundi langu na ndio maana nimekuja kusikiliza wana yapi ya kusema, lakini pia kusikia CHADEMA wanasema nini kuhusiana na nchi yetu.”

“kwa hivi sasa Mwanamke wa Tanzania anathaminiwa na kupewa haki kama Mwanamke na ndio lengo la Serikali yetu.”

“Natoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada na hatua zote zilizochukuliwa mpaka kufikia hapa na leo Mama yupo hapa na amekuwa Rais wa nchi.”

 

“Mimi Dada yenu na wenzangu wanaonisaidia tumefanya ubunifu wa kuhakikisha Taifa hili linaungana na kuwa moja. Tukaviambia vyama vya siasa vikae na kuja na namna wanataka tufanye nini.”

“Katika hilo chama chenu kikaja na maoni yake ya kutaka kisikilizwe peke yake na mimi nikamwambia Makamu wangu awaite watu wenu watano na upande huu watano mambo yakasonga mbele.”

Baada ya vikao hivyo leo mnamuona Rais amesimama kwenye jukwaa hili kuzungumza na Baraza la Wanawake la CHADEMA, jambo ambalo halikuwa rahisi huko nyuma ila kwa sababu ya ubunifu limewezekana.”

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply