The House of Favourite Newspapers

Julio Ataka Kumrithi Kahemele Simba

STORI: Na Said Ally | CHAMPIONI | Dar es Salaam

KOCHA wa zamani wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema yupo tayari kurejea kujihusisha na soka kwa mara nyingine baada ya kustaafu kwa muda kwa kuomba akabidhiwe majukumu ya ukatibu mkuu wa Simba.

Awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Patrick Kahemele ambaye aliamua kujiuzulu na kurejea Azam TV, hivi karibuni.

Julio aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba kwa nyakati tofauti, hivi karibuni alijiweka pembeni kujihusisha na masuala ya soka na kuikacha timu yake ya Mwadui baada ya kuchoshwa na maamuzi mabovu ya waamuzi wa ligi kuu.

Julio ameliambia Championi Jumatano kuwa, kwa upande wake hana wasiwasi endapo viongozi wa Simba wakiongozwa na rais wake, Evans Aveva wakiamua kumpa nafasi hiyo kwani anaamini anao uwezo.

“Siyo kama najipigia chapuo lakini kama viongozi wa Simba wakiamua kunipa nafasi ya

ukatibu sitaweza kukataa kwa sababu naipenda timu hiyo na kila mmoja anajua na kama nikiwepo naamini nitaongeza kitu fulani na kuifanya timu ipate matokeo mazuri.

“Uzuri ni kwamba sikufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na soka, hivyo hata nikirejea hakuna ambaye atashtuka na niwaahidi kwamba nitaitumikia nafasi hiyo kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa kipindi kirefu,” alisema Julio.

Save

Comments are closed.