The House of Favourite Newspapers

TOT vs E. Africa Taarab Valentine’s Day… Ni Vita ya Kopa vs Bi. Mwanahawa Dar Live

Malkia  wa Taarab, Khadija Kopa

STORI: NA MWANDISHI WETU | RISASI MCHANGANYIKO | DAR ES SALAAM

MACHO na masikio ya mashabiki wengi wa burudani hususan Muziki wa Taarab nchini wameelekeza ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar ambapo katika kusherehekea Sikukuu ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ wakali wawili, Malkia  wa Taarab atakuwa akipambana na Bi Mwanahawa.

ITAKUWAJE?

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, Bi Mwanahawa usiku huo atakuwa akiwakilisha bendi yake kongwe ya East Africa Melody huku Khadija Kopa akiiwakilisha TOT.

“Niwaombe tu mashabiki wa mirindimo ya Pwani tukutane usiku wa Februari 14 (Valentine’s Day) kuanzia saa mbili za usiku ndani ya kiwanja cha kijanja cha Dar Live kuwashuhudia wakongwe hawa wakitoshana nguvu vya kutosha,” alisema Mbizo.

Bi Mwanahawa.

ZITAKAZORINDIMA SASA

Mbizo aliongeza kuwa, usiku huo vibao vingi vitarindima ambapo kwa upande wa Khadija Kopa atashusha vibao vyake vyote vilivyowahi kubamba na ambavyo vinaendelea kubamba. “Kopa ataanza na Mjini Chuo Kikuu, Fahari ya Mwanamke, Nimpe Nani, Kadandie,

Magumegume na nyingine nyingi huku Bi Mwanahawa akirudisha mashambulizi kwa vibao vikali kama Wakerekwao, Wema na Roho Mbaya Haijengi,” alimaliza Mbizo.

SAPRAIZ KIBAO KUTOLEWA

Mbizo alimalizia pia kwa kapo 100 za kwanza watakaopendeza watapata sapraiz kibao ambayo imeandaliwa na ukumbi huo sambamba na huduma bora ya VIP.

“Siku zote Dar Live huwa tunajali mashabiki wote wa burudani. Mbali na uwepo wa nyama choma, fl at screen kila engo na red carpet safi ndani, usiku huo utakuwa wa kipekee kwa kuwapa kipaumbele kapo 100 wa kwanza watakaotoka chicha zawadi na pia huduma bora ya VIP.

“Wapendanao wote niwatoe pia wasiwasi, safu ya ulinzi imepangwa vizuri kwa hiyo si jambo la kuhofi a ndani ya kiwanja chetu hiki,” alipigilia msumari Mbizo.

Save

Save

Comments are closed.