The House of Favourite Newspapers

Juma Nyosso Kortini

 

MLINZI wa timu ya Kagera Sugar, Juma Said Nyosso anatarajiwa kupandishwa Mahakamani siku yeyote kuanzia leo (Jumanne), kutokana na kutenda kosa la jinai wakati akitoka nje ya uwanja.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, RPC Agustine Ollom amesema bado wanamshikilia mchezaji huyo wa Kagera na wakati watakapomaliza mahojiano naye wanatarajia kumpeleka Mahamakani kwa ajili ya mashtaka dhidi yake.

 

“Bado mtuhumiwa yuko mahabusu anaendelea kuhojiwa na yule majeruhi yupo hospitali kwa hiyo tunategemea madaktari wakatakavyo kuwa wamepita hii ’round’ ya asubuhi watatupa hali yake jinsi anavyoendelea. Juma Nyoso amefanya kosa la jinai hivyo sisi tutampeleka Mahakamani mapema itakavyowezekana na huko ndipo itakapojulikana kama alitenda kosa au laa na mwisho kutolewa adhabu juu yake”, alisema RPC Agustine Ollom.

 

Juma Said Nyosso alikamatwa jioni ya jana (Jumatatu) baada ya mechi kumalizika dhidi ya Simba katika dimba la Kaitaba ambapo wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanaelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa bahati mbaya mmoja ya mashabiki inasemekana alimpulizia vuvu zela Nyosso ndipo naye alipompiga shabiki huyo mpaka kupoteza fahamu.

Comments are closed.