The House of Favourite Newspapers

Juno Yatuma Picha ya Kwanza ya Jupita

0

JUNO 2

Muonekano wa picha ya kwanza ya Sayari ya Jupita.

Chombo cha anga za juu cha Shirika la Marekani la NASA kilichopewa jina Juno kimetuma picha za kwanza za Sayari ya Jupita.

Mojawapo ya picha hizo iliyotolewa na NASA jana Jumanne inaonesha sayari hiyo ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.

JUNO 1

Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede, mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani.

Picha hiyo ilipigwa Jumamosi wakati chombo hicho kilipokuwa kinaizunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.

Hata katika umbali huo, Shimo Jekundu, lililosababishwa na dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana.

Juno iliingia katika mzingo wa Jupita wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambayo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.

35F7BE5500000578-3674016-image-m-3_1467737614656

Wanasayansi wa Nasa wakishangilia baada ya Juno kuwasili kwenye Sayari ya Jupita.

Safari ya kifaa hicho kutoka duniani hadi Jupita ilichukua miaka mitano.

Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.

Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupita, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi ila baadaye vilifunguliwa.

Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupita zitapokelewa mwezi ujao na Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.

35F64E1A00000578-3674016-The_Juno_team_spoke_to_the_press_following_the_spacecraft_s_succ-m-2_1467702538865

Wanasayansi wa Nasa wakiongea na wanahabari baada ya Juno kutua Jupita.

Leave A Reply