The House of Favourite Newspapers

Jwtz Watangaza Kiama – ”Salimisheni Sare Za Jeshi Ndani Ya Siku 7 Kwenye Vituo Vya Polisi”- Video

0

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa ufafanuzi kwa jamii kuhusiana na kadhia inayokinzana na katazo la kisheria la raia kuvaa, kumiliki au kuuza mavazi ya kijeshi au yanayofanana na sare za kijeshi.

Taarifa iliyotolewa na JWTZ imeeleza kuwa jeshi linakataza kuvaa mavazi ya jeshi ambayo ni pamoja na kombati (vazi la mabaka mabaka), makoti, tisheti, suruali, magauni, kofia, viatu, mabegi na kaptula zenye rangi zinazofanana au kushonwa katika mitindo ya kijeshi.

Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano Makao Makuu ya Jeshi (JWTZ), Luteni Kanali Gaudentius Ilonda ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma mbele ya wanahabari, ambapo amesema katazo hilo la mavazi ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 iliyofanyika marejeo mwaka 2002.

Aidha Luteni Kanali Ilonda amesema Jeshi la Wananchi Tanzania linawasihi na kuwaomba wananchi kusalimisha mavazi hayo ndani ya siku saba (7) na baada ya siku hizo kuisha, atakayekutwa na mavazi hayo atachukuliwa hatua za kisheria

Hata hivyo Jeshi hilo linawafahamisha wananchi kuwa utekelezaji wa majukumu yake ya msingi na mengineyo unategemea sana ushirikiano mzurie wa wananchi wote.

Leave A Reply