The House of Favourite Newspapers

#GlobalMusic: Kaa Tayari Kuipokea Hii Mpya ’10 Fingers’ Kutoka Kwa AKA Leo – (BTS Video)

Kama wewe ni mdau wa South African Hip Hop na wasanii wake, basi hii ni kwa ajili yako. Ukimuweka AKA na ANATII kwenye chumba kimoja hiki ndio kinachotokea…

Rapper kutoka South Africa AKA na mkali mwingine wa muziki wa Hip Hip kutoka nchini humo ANATII wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha video ya collabo yao mpya ’10 Fingers’ inayotarajia kutoka leo.

Kupitia channel yake ya YouTube, AKA ameamua kushare na mashabiki wake dakika 5 za behind the scenes ya video hiyo mpya. Ndani ya video hii utawaona rappers hao wakishoot video yao nzima ndani ya locations mbili tu, moja ikiwa kwenye setup ya studio na nyingine wakiwa nje ya mazingira ya studio. 

Itazame Behind The Scenes ya ’10 Fingers’ hapa chini.

Licha ya hayo, kikubwa nilichokigundua ndani ya visuals hizi ni uwepo wa mpenzi wa AKA, Bonang Matheba japo sina uhakika sana kama mwanadada huyo atakuwepo kwenye video hii itakapotoka hapo badaae ila kama wewe ni mashabiki wa mastaa hawa tegemea kuona kitu chochote.

Kaa karibu na sisi ili uwe wa kwanza kuicheki video hii itakapotoka rasmi hapo badaae.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

 

Comments are closed.