The House of Favourite Newspapers

Kadima Kabangu Amalizana na Simba

0

MSHAMBULIAJI wa DC Motema Pembe ya DR Congo, Kadima Kabangu, amefunguka kuwa tayari ameshamalizana na Simba na wiki hii kila kitu kitakuwa sawa tayari kwa kutangazwa kuwa mchezaji rasmi wa klabu hiyo.

 

Kwa muda mrefu, mshambuliaji huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba ambapo kwa sasa dili lake limeonekana kukamilika.

 

Tayari kikosi cha Simba kimeelekea Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao wa 2021/22 ambao watakuwa na kibarua kizito cha kutetea mataji yao, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam ambayo wameyachukua msimu wa 2020/21.

 

Pia timu hiyo ina kibarua cha kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, huku ikiwa na kumbukumbu ya msimu wa 2020/21 kuishia robo fainali.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kadima alisema kwa sasa meneja wake yupo Tanzania akifanya mazungumzo ya mwisho ya kumalizana na Simba.

 

“Meneja wangu yupo Tanzania kwa sasa, amesema kuwa wiki hii kila kitu kitakuwa sawa. Mimi nimeambiwa wiki hii nitasafiri kuja huko kukamilisha kila kitu, hivyo nasubiri taarifa hiyo, ni uhakika nakuja”.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply