Tanzia: Milionea Manga wa Gold Crest Afariki Dunia

 

Mfanyabiashara maarufu wa Madini na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Arusha ambaye pia ni mmiliki wa Hotel za Gold Crest zilizopo Mwanza na Arusha, Mathias Manga amefariki dunia muda mfupi uliopita nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

Aliywahi kuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ameandika kupitia akaunti yake ya Twitter….

 

“RIP Mathias Manga: Nimehuzunika sana. Siamini rafiki yangu umetangulia: Mtu mwema,mwenye roho nzuri na upendo, mkarimu, mwenye kujitoa kwa ajili ya jamii na watu. Mwenyezi Mungu akupe pumziko la amani. Pole kwa familia, ndugu na marafiki wote.”


Toa comment