The House of Favourite Newspapers

Kagame Aidhamini Arsenal

Wachezaji wa timu ya Arsenal.

RWANDA imeingia mkataba wa miaka mitatu na Arsenal ambapo kwenye mabega ya jezi zao kutakuwa na ujumbe wa ‘Visit Rwanda’.

Ujumbe huo ambao unamaanisha tembelea Rwanda, utakuwa kwenye jezi za kikosi cha kwanza pamoja na timu ya vijana na ile ya wanawake ya klabu hiyo.

Vinal Venkatesham, ambaye ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Arsenal amesema kwamba ; “Huu ni ubia mzuri ambao utasapoti Rwanda kutangaza utalii wake.”

Mkataba huo pia utahusisha kikosi cha Arsenal kutembelea Rwanda na kuweka kambi pamoja na makocha wao kuendesha kozi mbalimbali kwa maendeleo ya soka la nchi hiyo.

Comments are closed.