The House of Favourite Newspapers

Mhariri Mkuu Gazeti la Xinmin la China Atembelea Global Group

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akiongea na  Mhariri Mkuu wa Gazeti la Xinmin  Evening News, Dr Justin Qiu (katikati) wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu ajulikanaye kwa jina la utani la Juma Sharobaro.

MHARIRI Mkuu wa gazeti la XINMIN EVENING NEWS la China,  Dr Justin Qiu leo ametembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanyika katika ofisi hizo.

Dr Justin Qiu akiendelea kuongea na  Mrisho (hayupo pichani).

Mhariri huyo amefika katika ofisi za Global Group majira ya asubuhi akiwa ameambatana na wafanyakazi  wenzake  wawili kutoka gazeti la XINMIN na mwenyeji wao wa hapa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu ‘Juma Sharobaro’.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abadallah Mrisho,  aliwaeleza jinsi magazeti ya kampuni hiyo yanavyotayarishwa na kupelekwa sokoni huku pia akiwajulisha kazi za Global Digital inayojumuisha website ya Global Publishers na Global TV Online.

Dr Qiu akipokea zawadi kutoka kwa Mrisho.

Dr Justin na wenzake wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata na kuahidi kuendelea kushirikiana na Global Group katika masuala mbalimbali katika tasnia ya uchapishaji wa magazeti. Xinmin ni gazeti linalotoka kila siku kwa lugha ya kichina na linachapa nakala milioni moja kwa siku, lilianzishwa miaka 90 iliyopita!

Picha pamoja ya wageni na mwenyeji wao.
Dr Qiu akiweka saini kwenye kitabu cha wageni.

 

Comments are closed.