The House of Favourite Newspapers

Kagera Yatoa Baraka Kwa Mbaraka Kukipiga Azam FC

0
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, akiongea na wanahabari leo.

KLABU ya Azam FC leo imekubaliana na Klabu ya Kagera Sugar ambapo imeruhusiwa kumchukua mchezaji Mbaraka Yusuph kuichezea timu hiyo ya jijini  Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari  wa Azam, Jaffar Idd, meeleza kuwa timu hiyo ilimsajili mchezaji huiyo  kutoka Kagera Sugar kwa kufuata taratibu zote za usajili, huku akidokeza kuwa tayari Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeidhinisha usajili wake kupitia mfumo mpya wa usajili wa kimtandao wa TMS.

…Akionyesha barua ya timu ya Kagera Sugar kukubali kumuachia Mbaraka Yusuph.

Baada ya kikao  cha jana makao makuu ya Azam kilichofanyika jana,  Kagera Sugar walitoa rukhsa  kwa aliyekuwa mchezaji wao huyo kuchezea Azam.

STORI: MUSA MATEJA/GPL

Leave A Reply