Kagere ataka mabao 30 Simba

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere

BAADA ya kufunga mabao 20 mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara, mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa mabao hayo hayatoshi kwani anataka kufunga mabao zaidi ya 30.

 

Idadi hiyo ya mabao 30 na kuendelea inafananishwa na idadi ya mabao aliyofunga Mohammed Salah wa Liverpool msimu wa 2017/2018 ambapo alifi kisha 32 na kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England.

 

Kagere katika mechi tano ambazo Simba imebaki nazo, anatakiwa kufunga mabao 12 ili kuifi kia rekodi hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kagere alisema kuwa anatamani afunge zaidi ili kuisaidia timu yake ichukue ubingwa na kwa mabao 30 na kuendelea anaona yatafaa kuipa ubingwa Simba.

 

“Hesabu zangu katika michezo mitano iliyobaki ni kufunga mabao 12, yataisaidia sana Simba kuwa bingwa sasa, nina mabao 20, nikifunga mengine 12 nitakuwa nimefi kia idadi ambayo ninahitaji ya mabao 32,” alisema Kagere.

STORI NA MARCO MZUMBE, CHAMPIONI JUMATANO

KOCHA ZAHERA Awahoji Waandishi, Awauliza Kuhusu SIMBA!


Loading...

Toa comment