The House of Favourite Newspapers

KAHABA KUTOKA CHINA-07

0

Bwana Shedrack akajiona kumaliza kila kitu, kitendo cha yeye kuchukua simu ya Rose na kisha kuanza kukaa nae aliona kwamba hiyo ingempa unafuu kutokana na tabia ambayo alijua kwamba Rose alikuwa ameianza, tabia ya kutoka nje ya nyumba na kisha kuonana na wanaume. Simu akawa nayo yeye, kila meseji ambayo ilikuwa ikitumwa, alikuwa akizipuuzia kwa sababu zilikuwa zikitoka katika namba ngeni kabisa.
Katika kipindi hicho ndicho ambacho alikuja kugundua kwamba binti yake alikuwa mwaminifu sana na hakuwa na habari na mwanaume yeyote yule. Malalamiko ya wanaume ambao walikuwa wamekataliwa yakamfanya kufurahia sana kwa kuona kwamba binti yake hakuwa mtu wa kupenda wanaume kama ambavyo alifikiria kabla.
“Huyu ndiye binti anayetakiwa kuishi nami kama mwanangu. Ila huyu mtu…huyu…Mhh! Sijui” Bwana Shedrack alikuwa akijiseme katika kila kipindi ambacho alikuwa akiangalia meseji ambazo zilikuwa zikitumwa katika simu ya Rose.
Kuna mtu mmoja tu ambaye alikuwa akimhofia sana juu ya binti yake, mtu huyu kila wakati alikuwa akituma meseji za mapenzi, meseji ambazo alikuwa akizituma yeye hazikuwa za kulalamika au za kumtaka Rose kimapenzi bali meseji ambazo alikuwa akizituma yeye ni zile ambazo zilionyesha kwamba walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi fulani.
Bwana Shedrack akashikwa wasiwasi sana na mtu huyu kwa kuona kwamba angeweza kuleta mambo fulani hapo baadae. Kila alipokuwa akiliangalia jina la mtu huyo, Joshua, moyoni mwake alikuwa akikosa amani na kukereka sana.Tayari alikuwa amekwishaanza kuhisi kitu lakini kutokana na ukaribu ambao alikuwa ameuweka kwa binti yake pamoja na kumbana kupita kawaida, aliona kila dalili kwamba mwanaume huyo asingeweza kupata nafasi.
Bwana Shedrack hakutaka kubaki hivi hivi tu bila kufanya chochote kile, alichokifanya ni kuhakikisha kwamba Peter anapata nafasi kubwa zaidi ya kuwa na binti yake. Mara kwa mara Peter alikuwa akifika ndani ya nyumba hiyo, alikuwa akiongea sana na Rose na mwisho wa siku kuwa wapenzi ambao walitegemea kuoana na kuwa mume na mke.
Hiyo ndio ikaonekana kuwa furaha kwa Bwana Shedrack, kile ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo kikaonekana kukamilika bila matatizo yoyote yale. Kitendo cha Peter kuanza mahusiano na binti yake kikaonekana kumpa amani. Japokuwa kila kitu kilikuwa kimekamilika lakini hakutaka kumrudishia simu ile kwa kuona kwamba Joshua, mwanaume ambaye alikuwa akituma sana meseji za kimapenzi angeweza kuharibu kila kitu.
Kila siku alikuwa na simu ya Rose chumbani kwake, hakutaka kuiacha mbali, alikuwa akikaa nayo karibu huku muda mwingi akizisoma meseji ambazo walikuwa wakizituma wanaume mbalimbali ambazo kwake zikaonekana kuwa kama kichekesho vile.
“Binti yangu hamuwezi kumpata kirahisi” Bwana Shedrack alikuwa akijisemea huku akiwa amekenua meno yake.
“Yule ni mtoto wa mwanajeshi, ana kila ulinzi mahali hapa. Ila huyu Joshua nae ananichanganya sana. Hivi hizi meseji zake mbona zipo tofauti na wengine? Yaani yeye anaziandika kimapenzi zaidi, au kashamchukua binti yangu? Hapana. Hebu ngoja nichunguze” Bwana Shedrack alikuwa akijisemea kila alipokuwa akiziangalia meseji ambazo Joshua alikuwa akiendelea kuzituma ndani ya namba ile.
Siku zikakatika kama kawaida mpaka siku ambayo aliisikia simu ya Rose ikianza kuita. Alichokifanya, kama kawaida yake akaichukua simu ile na kisha kuangalia jina la mpigaji, haikuwa namba ngeni, ilikuwa ni simu kutoka kwa Irene huku namba ikiwa imehifadhiwa kama ‘My Hubby Irene’.
Kwanza Bwana Shedrack akashtuka kidogo, namna ya jina lile lilivyokuwa limehifadhiwa ndani ya simu ile likaonekana kumtia wasiwasi kupita kawaida. Hakutaka kujipa sana presha kwani alikwishasikia kwamba wanawake huwa wanayahidhi majina ya wanawake wenzao kwa namna ambayo mwanaume hawezi kutumia kulihifadhi jina la mwanaume mwenzako. Akakibonyeza kitufe cha kijani na kisha kuipeleka simu sikioni.
“Ndio umefanya nini sasa?” Sauti ya Irene ilisikika simuni na kuendelea huku Bwana Shedrack akibaki kimya.
“Nakuuliza wewe. Ndio umefanya nini tena mpenzi. Yaani mahaba yote ambayo nilikupa kitandani, yaani kuyacheza matiti yako yote mpaka mtoto wa kike kulegea kitandani, eti leo hii unakubali kuolewa na mwanaume, au haujui kwamba mimi ndiye mwanaume wako? Au haujui kwamba mimi ndiye mtu ambaye nimekutoa bikira kwa kutumia kiungo wa bandia? Hivi kwa nini unaamua kunisaliti Rose? Hivi kwa nini umeamua kufanya jambo kama hili kwangu. Au mjomba kakulazimisha? Na kama alikulazimisha kwa nini usiongeondoka nyumbani ukaja japo huku hosteli ukaja tukakaa pamoja? Umenikasirisha mke wangu, mahaba yangu yameonekana kuwa si kitu” Irene aliongea kwa sauti ya hasira huku Bwana Shedrack akiwa kimya akimsikiliza tu bila kuongea chochote kile.
“Umenikasirisha…umenikasirisha sana…umenisikia..halllow” Sauti ya irene iliita kwa hasira na kuita baada ya kutokuisikia sauti ya Rose.
“Hallow. Endelea nakusikiliza” Bwana Shedrack aliitikia na ghafla simu kukatwa.
Bwana Shedrack akabaki akitetemeka kwa hasira, tayari akaonekana kubadilika kupita kawaida, akakunja ngumi na kisha kuupiga ukuta kwa hasira. Maneno ambayo alikuwa ameyasikia kutoka kwa Irene yakaonekana kumkasirisha kupita kawaida. Akaanza kuliangalia tena jina la Irene, akapata jibu ya namna ambavyo jina lile lilikuwa limehifadhiwa ndani ya simu ile.
Mwili ulikuwa ukitetemeka kwa hasira, kijasho chembamba kikaanza kumtoka huku akiwa amekunja ndita kwa hasira. Hakutaka kubaki chumbani, alichokifanya ni kutoka na kuelekea sebuleni. Furaha yote ambayo alikuwa nayo ikawa imemtoka, hakuamini kama msichana Irene ambaye alikuwa amemleta ndani ya nyumba yake alikuwa msagaji na ambaye alikuwa akimsaga binti yake, Rose.
“Haiwezekani. Irene msagaji!” Bwana Shedrack alikuwa akijisemea kwa hasira.
Kila kitu ambacho alikuwa akijiuliza mahali hapo alikosa jibu kabisa, hakuamini kama kweli Irene alikuwa msagaji. Huku akiwajifikiria jambo hilo, akapata jibu juu ya hali ya mapokezi makubwa ambayo Rose alimpokea Irene katika kipindi ambacho alikuwa amefika nyumbani hapo kwa mara ya pili mara baada ya kutoka chuo, hakuishia hapo tu bali akapata jibu juu ya sababu iliyowafanya wawili hao kuchukua muda mrefu kujifungia chumbani.
“Nitaua mtu” Bwana Shedrack alijisema.
Wala hazikupita dakika nyingi, akasikia muungurumo wa gari kutoka nje, akasimama na kisha kuchungulia, lilikuwa gari la Peter na kisha Irene kuteremka. Bwana Shedrack akajikuta akishikwa na hasira zaidi, hata Rose alipoingia ndani ya nyumba hiyo, bado hasira zake zilionekana kuwa waziwazi.
“Kuna nini tena baba?” Rose aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Irene……!” Bwana Shedrack alisema huku akiobnekana kuvimba kwa hasira na kuiweka simu ya Rose mezani kitendo ambacho kilimshtua sana Rose.
Alipoiweka simu ile mezani, kwa haraka sana akamwangalia Rose machoni ili kuona angeonyesha hali gani. Alipomuona Rose ameshtuka, akajua kwamba kile ambacho alikuwa kikihisi kilikuwa chenyewe, hakuwa amebahatisha. Rose akabaki kimya, kwa mbali akaonekana kutetemeka kupita kawaida, alitamani kuichukua simu ile na kisha kuondoka nayo lakini akajikuta akikosa nguvu, akajiweka kochini.
“Niambie kuhusu mahusiano yako na Irene” Bwana Shedrack alimuuliza Rose.
“Ni ndugu yangu” Rose alijibu.
“Usitake kunikasirisha. Niambie mahusiano yako na Irene” Bwana Shedrack aliuliza kwa hasira huku akionekana kuanza kubadilika.
Rose hakujibu kitu, hakuwa tayari kumwambia baba yake kwamba Irene alikuwa msichana ambaye alikuwa akimsaga kila siku chumbani, hakuwa radhi kumwambia kwamba Irene alionekana kuwa kama mume wake wa ndoa kutokana na kufanya mambo mengi ambayo wanandoa hufanya chumbani.
“Umeanza lini usagaji?” Bwana Shedrack alimuuliza Irene.
“Nisamehe baba”
“Hilo si jibu ninalolitaka. Nimekuuliza umeanza lini usagaji? Sijauliza kuhusu msamaha hapa” Bwana Shedrack alimuuliza Rose huku akionekana kukasirika kupita kawaida.
“Irene alikuwa akinilazimisha”
“Alikuwa akikulazimisha! Kukulazimisha kivipi na wakati inaonyesha kabisa kwamba nyie ni wapenzi, tena wapenzi waliokubuhu” Bwana Shedrack alimuuliza Rose.
“Nisamehe baba” Rose alisema huku akianza kuomba msamaha.
“Yaani mwanajeshi mimi shupavu eti leo nimezaa mtoto msagaji, yaani hii skendo hata wanajeshi wenzangu wakisikia, watanishangaa sana” Bwana Shedrack alimwambia Rose.
Rose akaanza kulia, moyo wake ukaanza kuumia hasa mara baada ya kuona kwamba hata baba yake alikuwa amekwishajua kwamba alikuwa msagaji. Akaendelea kuomba msamaha zaidi na zaidi lakini Bwan Shedrack hakutaka kuelewa kabisa, katika kipindi hicho, alikuwa akijitahidi kuzungumza maneno mengi ambayo aliamini kwamba yangemchoma Rose moyoni.
“Yaani unataka kuniambia kwamba vidole vya msichana mwenzako vinakuridhisha, yaani unataka kuniambia kwamba unachukua muda wako kuunyonya mdomo wa msichana mwenzako! Hivi hauoni kwamba huo ni uchafu, hivi hauoni kufanya mapenzi na mwanamke mwenzako ni uchafu, uchafu uliokithiri, uchafu ambao hata Mungu haupendi kabisa. Hivi mna tofauti gani na mashoga, hivi mnatofauti gani na wale watu wa jinsia moja ambao wanakwenda kanisani na kutaka kufunga ndoa ya jinsi moja? Nisikilize Rose, sikuwa nikikufungia ndani ili uwe msagaji, nilikuwa nakufungia ndani kwa sababu nilitaka uwe binti mzuri zaidi ya ulivyokuwa. Hiyo ndio ilikuwa maana yangu kubwa. Badala ya kuwa binti mzuri zaidi, umekuwa zaidi ya binti mbaya, sasa kazi yote ambayo nilikuwa nikiifanya ikaonekana kuwa ni bure kabisa. Yaani ni bora, ni bora ungefanya mapenzi na wanaume wote wanaokutaka hapa Magomeni kuliko kufanya mapenzi na msichana mwenzako. Acha nikwambie Rose, sitaki kuyafuatilia maisha yako, sitaki kumwambia mtu yeyote juu ya uchafu wako, nakuachia wewe na mume wako mtarajiwa. Akijia kufahamu, mtajijua kivyenu. Kwa huyu mshenzi mwenzako, nitamuua, nakwamba kwamba NITAMUUA. Haijalishi atakimbia nchini Tanzania au la…NITAMUUA” Bwana Shedrack alimwambia Rose, akachukua simu ile aliyoiweka mezani na kisha kuondoka mahali hapo.
Rose akabaki akilia tu, hakuamini kama baba yake, Bwana Joshua alikuwa amefahamu kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Hakunyamaza, aliendelea kulia zaidi na zaidi. Kuanzia siku hiyo, akawa tu wa kulia kila siku, moyo wake ukapoteza furaha, kila alipokuwa akimwangalia baba yake, alikuwa akijisikia aibu, moyo ulikuwa ukimsuta kupita kawaida.
Siku zikaendelea kukatika kama kawaida. Rose hakutakiwa kutoka nje ya nyumba hiyo, hata katika kipindi ambacho Peter alikuwa akifika mahali hapo kwa ajili ya kumchukua Rose, alikuwa akizuiliwa. Lengo kubwa ambalo alikuwa amelipanga Bwana Shedrack ni kumuua Irene ambaye kwake alionekana kuwa msichana mmoja mbaya ambaye hakutakiwa kuishi katika dunia hii.
Alihofia kwamba kama angeruhusu Rose kutoka nje ya nyumba hiyo, basi angeweza kutumia simu kumtaarifu Irene juu ya uamuzi ambao alikuwa ameupanga baba yake juu yake. Hata Peter alipokuwa akifika mahali hapo, alikuwa akiongea na Rose huku Bwana Shedrack akiwa pembeni yake.
Baada ya kipindi fulani, hali ya Rose ikaanza kubadilika, akaanza kujisikia uchovu, muda mwingi akawa akitamani kulala na kilipofika kipindi fulani kuanza kutapika. Dalili zote za mwanamke mjauzito zikaanza kuonekana mwilini mwake. Hali hiyo haikujificha, John akamwambia baba yake, Bwana Shedrack ambaye akaamua kumuita Rose.
“Una mimba?” Bwan Shedrack alimuuliza Rose.
“Ndio”
“Ya nani?”
“Ya Peter.
“Safi sana. Bora muoane tu”
Mimba ile ikaonekana kuwa sababu, mipango ya harusi ikaendelea kuchangwa kwa kasi, watu wakazidi kupewa taarifa juu ya harusi hiyo kiasi ambacho kilionekana kuwafurahisha wazazi wa pande zote mbili.
Bado dukuduku la kutaka kumuua Irene lilikuwa likiendelea moyoni mwake, kila alipokuwa akimwangalia Rose mawazo yake yalikuwa yakimfikiria Irene ambaye alionekana kumharibu mtoto wake. Siku ambayo aliipanga kuwa siku maalumu ya kumuua Irene ikawadia, alichokuwa amekiamua ni kumfuata Irene usiku na kisha kumuua katika kifo ambacho kingetangazwa kufanyika katika mazingira ya kutatanisha.
Rose akaonekana kuhisi kitu, siku hiyo baba yake akaonekana kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa, toka alipokuwa amerudi kutoka kazini, hakuonekana kama alikuwa wa kawaida kama siku nyingine, kila alipokuwa akimwangalia, aligundua kwamba kulikuwa na kitu.
Ilipofika saa mbili kasoro usiku, Bwana Shedrack akaondoka mahali hapo huku bunduki yake ikiwa kiunoni. Macho ya Rose yalipotua katika bunduki ile iliyokuwa kiunoni, hakutaka kujiuliza, tayari alijua kwamba baba yake, Bwana Shedrack alikuwa akiondoka kuelekea katika hosteli aliyokuwa akiishi Irene kwa lengo la kumuua.
“Leo ndio siku yake” Bwana Shedrack alijisemea huku akiingia ndani ya gari huku akionekana kuwa na hasira na kisha kuondoka mahali hapo huku akimuacha Rose akiwa hajui afanye nini.

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Alhamisi hapahapa.

Leave A Reply