The House of Favourite Newspapers

KAJALA ACHARUKA MWANAYE KUKUZWA UMRI

Kajala Masanja

MSANII mwenye mvuto wa aina yake Bongo Muvi, Kajala Masanja amesema hana muda wa kubishana na watu wa mitandaoni kuhusu umri wa mtoto wake Paula kwani yeye ndio mzazi na si mtu mwingine. Akizungumza na Amani hivi karibuni mara baada ya kumposti mwanaye huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumpongeza kufikisha miaka 16, Kajala alisema ameshangazwa na watu walioanza kumsema mwanaye kuwa ana zaidi ya miaka 16.Picha inayohusiana

“Mimi naona kubishana na watu wa Insta ni kujisumbua kwa sababu mtoto nimemzaa mwenyewe lakini wanaibuka watu wanajifanya wanajua umri wake kuliko mimi, basi waendelee kuamini ni mkubwa zaidi,” alisema Kajala. Mtoto huyo Kajala amezaa na prodyuza wa Bongo Fleva, Paul Matthysse ‘P Funk’ ambaye walishamwagana kitambo.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Comments are closed.