KAJALA AKESHA AKIMSALIA PAULA

MSANII kutoka Bongo Movie, Kajala Masanja amefunguka ya moyoni kuwa anapitia wakati mgumu katika malezi ya mtoto wake, Paula kutokana na kusifiwa uzuri hivyo anaogopa atawahi kuharibikiwa hadi inafikia kipindi anakesha anasali kwa ajili yake.

Akizungumza na Za Motomoto, Kajala alisema kwa sasa anapitia wakati mgumu sana kumlea mtoto huyo kwani kila siku zinavyozidi kwenda uzuri wa mtoto wake unazidi kuongezeka watu wanamsifia hadi anakosa mawazo sana.

“Kila nikimuangalia Paula naona nina kazi nzito sana ya kumlinda maana kila mtu anamsifia mzuri ana umbo zuri mpaka imefika wakati naogopa sasa nasali sana kwa ajili yake. Hata huko shule ninakompeleka kwa vile ndio kuna ulazima ila natamani nimfungie ndani tu magume gume wasimuone,” alisema Kajala.

Na Imelda Mtema

Toa comment