The House of Favourite Newspapers

Kajala Amuanika Mrithi Wa Harmo

0

IKIWA ni mwezi mmoja tu umepita tangu Couple maarufu ya mastaa kutoka kiwanda cha Bongofleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ na Bongomuvi  Kajala Masanja kuvunjika kwa aibu, mlimbwende huyo amemuanika mpenzi wake mpya ambaye ndiye mrithi wa Harmo.

Kajala ambaye amekuwa tishio kwa umbo matata linalowatoa udenda midume hapa Bongo, amemuibua jamaa kutoka Nigeria ambaye ni muigizaji na kuandika ujumbe mzito uliopigia mstari kuwa wawili hao ni wapenzi kwa sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kajala aliposti picha ya kijana huyo aliyezaliwa mwaka 1984, na kushusha ujumbe huu mwanana ’Yeah it’s my baby’s birthday wish you a good health and more years to come happy birthday NAKUPENDA @kingwoleojo @kingwoleojo ❤’

Kingwoleojo ambaye jina lake kamili ni Wole Ojo naye alijibu ‘Thanks love ❤️❤️❤’.

Cc: mushigabriel

Leave A Reply