The House of Favourite Newspapers

Kajala, Harmo Penzi Lao Gumzo Mjini

0

UNAWEZA ukasema gari kwa sasa limewaka! Mwanamama Kajala Masanja na mpenzi wake Rajabu Abdul ‘Harmonize’ wamezidi kuoneshana mahaba niue laivu kila kukicha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye sherehe ya kumtambulisha First Lady kutoka Lebo ya Konde Gang Music World Wide, Anjella Tz, juzi Alhamisi, Kajala aliposti picha akiwa na Harmo na kuandika maneno yaliyosomeka:“Mama na baba Anjela.

 

”Jambo hilo lilileta mjadala kwa mashabiki, huku baadhi yao wakimponda Kajala na wengine wakionekana kumpongeza.“

Huyu naye anajishaua anajifanya kama hapo kwa Harmo kafika eti mama na baba Anjella, mwanao ni huyo Paula ambaye hana adabu kwanza muache dada wa watu usije mtia nuksi bure kama za Paula,” alichangia shabiki mmoja mtandaoni.

 

Wengine walionekana kumpongeza kwa kile alichokifanya:“Hongera yako mama naona maisha yanakunyookea hapo naamini Anjella yuko mikono salama kabisa Mungu azidi kuwaweka, naipenda sana couple yenu,” aliandika shabiki mwingine aliyejulikana kwa jina la Kika.

 

Kwenye hafla ya kumtambulisha Angella, Harmo alionekana kukaa beneti na Kajala huku ‘wakinyonya’ mvinyo kwa raha zao.

Kuna wakati wawili hao walicheza pamoja, wakati mwingine walipokuwa wamekaa, walishikana kimahaba.

 

Wawili hao wamekuwa wakieleza ni jinsi gani walivyozimikiana na kwamba wako tayari kwa ajili ya kwenda kwenye neksti levo ya penzi lao kwa maana ya kufunga ndoa huku Harmo akikiri kwa kinywa chake kwamba siku Kajala akimuuacha atakufa.

Imeelezwa kuwa, Kajala amekuwa akimdekeza na kumpetipeti Harmo kama mfalme kiasi cha kumfanya kumsahau aliyekuwa mkewe, Muitaliano Sarah.

 

TUJIKUMBUSHE

Kajala alinasa moyoni mwa Harmo miezi michache iliyopita baada ya Harmo kumwagana na aliyekuwa mkewe Sarah na sasa penzi lao limekuwa gumzo mjini.

Leave A Reply