The House of Favourite Newspapers

Kajala Masanja: Nilifunga Kumuombea Sonia Ukraine

0

KAJALA Masanja au Frida Kajala; ni staa mkubwa wa Bongo Movies ambaye amemshukuru Mungu baada ya Watanzania waliokuwa nchini Ukraine kufanikiwa kuondoka kutokana na vita akiwemo mtoto wa mwigizaji mwenzake, Monalisa aitwaye Sonia.

 

Kajala anasema kuwa, alifunga na kumuombea Sonia ambaye alikuwa masomoni nchini huo ili aweze kuyapita yote ambayo alikuwa akiyapitia na hatimaye aweze kurudi nyumbani salama na kuungana na familia yake tena na kweli Mungu ametenda kwa hilo kwani mtoto huyo ni miongoni mwa Watanzania waliofanikiwa kunusurika kwa kuondoka nchini Ukraine.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Kajala anasema kuwa, kilikuwa ni kipindi kigumu mno alichokuwa anapitia Monalisa na yeye kama mzazi anajua ni machungu gani alikuwa anapitia.

 

Kajala anasema kuwa, kazi yake kubwa ilikuwa ni kumuombea kila siku ili aweze kurejea nyumbani salama.

“Kwa kweli kama mzazi, ilikuwa ni lazima ujisikie vibaya na uchungu hivyo nilifunga na kumuombea sana ili Mungu amlinde na ninaamini kabisa Mungu ametenda,” anasema Kajala ambaye siku hizi mashabiki wake wanapenda kumuita Mama Paula

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply