The House of Favourite Newspapers

Kajala: Naangalia Zaidi Furaha Yangu Kuliko Kitu Chochote Msinipangie Maisha!

0

 

Kajala Masanja au Mama Pau.

 

Kajala Masanja au Mama Pau; ni staa mkali kwenye kiwanda cha filamu nchini Tanzania almaarufu Bongo Movies ambaye anasema kwamba, kitu pekee anachokiangalia zaidi kwa sasa kwenye maisha yake ni furaha yake ambayo ni muhimu kuliko makelele mengi ya waja yanayosikika kwenye mitandao ya kijamii.

 

Kumekuwa na kelele nyingi kutokana na kitendo cha kukubali kurudiana na ex-wake, Harmonize kwa kuwa kuna upande haukutaka hilo litokee.

 

Lakini Kajala anasema kuwa, ameamua kujipa furaha kwani hahitaji kujipa stresi wakati wote.

Harmonize.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Kajala au Fridah anasema kuwa, watu wanaweza wasimuelewe harakati zake, lakini ukweli ni kwamba kwenye maisha yake anaangalia zaidi ni nini ambacho anakifurahia na si watu wanachopenda yeye afanye, hicho ndicho kitu anachokiangalia zaidi kwa sasa.

 

“Mimi naangalia zaidi furaha yangu kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yangu hivyo ni vigumu sana mtu kunipangia furaha yangu iweje. Hapo ndipo watu wanashindwa kuelewa,” anasema Kajala ambaye kwa sasa anainjoi maisha ndani ya Konde Village pale nyumbani kwa Harmo au Konde Boy.

STORI NA SIFAEL PAUL

KAJALA na HARMONIZE Wakiwa GYM, WAACHIA PICHA ya UTATA, PENZI LIMEKOLEA..

Leave A Reply