The House of Favourite Newspapers

KAJALA: SIO WAKATI WA KUMBEZA WEMA

Kajala Masanja

STAA anayefanya vizuri Bongo Muvi, Kajala Masanja amefunguka kuwa huu si wakati wa kushangilia kilichomtokea msanii mwenzake ambaye pia alikuwa rafiki yake wa karibu, Wema Sepetu bali inapaswa kumpa moyo na kuwa naye karibu.

Akizungumza na Ijumaa kuhusu suala la kuvuja kwa video za Wema na mpenzi wake aitwaye Patrick Christopher ‘PCK’ wakiwa faragha, Kajala alisema kuwa kila binadamu anakosea kwa sababu hawezi kuwa mkamilifu katika maisha yake yote hivyo kukosea ni jambo la kawaida hivyo anampa moyo Wema, asijione mkosefu sana na kukata tamaa ya kuendelea kufanya kitu chochote.

 

“Sioni kama ni sawa kila mmoja kumuona Wema kama ni mkosefu kupitiliza kwa sababu najua wazi hakuna aliye mkamilifu hata kidogo na siku zote kuteleza sio kuanguka ni wakati tu wa kumpa moyo na kuwa naye karibu,” alisema Kajala.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.