Kajifungua, Anasumbuliwa Na Michirizi Tumboni, Afanyeje?

HABARI mtaalam, binti yangu hivi karibuni amejifungua lakini tatizo kubwa linalomkosesha amani ni kutokwa na michirizi mingi tumboni. Nawezaje kumsaidia ili aondokane na tatizo hilo?

Mama Fauzia wa Kinondoni, Dar

Pole mama Fauzia kwa kuteswa na tatizo la binti yako. Ili aondokane na tatizo hilo kuna njia mbalimbali, miongoni mwazo ni kwa kutumia:

Mafuta ya mzaituni

Mshauri apake mafuta ya mzaituni kuanzia kwenye hipsi mpaka tumboni. Mafuta haya yanasaidia damu kutembea vizuri katika mfumo wake na kumuepusha na michirizi.

Mafuta ya mrujuani

Atumie mafuta haya kufanya masaji kwenye tumbo lake, hips pamoja na matiti.

Mafuta ya pamba

Achukue mafuta ya pamba, apake kwenye tumbo lake mpaka kwenye hips, mafuta haya pia yanasaidia kuondoa michirizi.

Mafuta ya samaki

Kwa kutumia mafuta haya alifanyie tumbo lake masaji. Inaelezwa kuwa wengi waliotumia mafuta haya wameona matokeo chanya.

Mkojo wa asubuhi

Ili kukomesha kabisa michirizi baada ya kujifungua, wakati una mimba ukiamka asubuhi hakikisha unachukua mkojo wa kwanza unapaka tumbo lote.

 


Loading...

Toa comment