The House of Favourite Newspapers

Kamala Harris: Marekani Kusaidia Tanzania Upatikanaji wa Huduma ya Intaneti ya Garama Nafuu

0

MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, leo Machi 30, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam amesema Serikali yake kupitia Idara ya Biashara na Maendeleo ya Marekani (USTDA) itasaidia katika kukamilisha suala la upatikanaji wa huduma ya Intaneti ya garama nafuu katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kupitia ruzuku ya Dola za Kimarekani milioni 1 kwa ajili ya kufanya utafiti na upembuzi yakinifu kusaidia kuanzishwa kwa mkongo mpya wa Mawasiliano.

Pia, itajenga Miundombinu kuwezesha upatikanaji wa Huduma za Kimtandao katika Nchi za Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda.

Pia, Marekani watejenga Kiwanda kitachenjua Madini ya Nickel na Madini mengine muhimu yanayochimbwa Tanzania, kikilenga kuzalisha Nickel iliyotayari kutengenezea betri kwa ajili ya kupelekwa Marekani na Soko la Kimataifa ifikapo Mwaka 2026

Ubia huu utafanya kazi ya kutafuta fursa za ziada katika kanda kwa ajili ya kupata Madini mengine muhimu ya kuchenjua katika Kiwanja hicho kipya. LifeZone Metals itaanzisha Kiwanda hicho mahali ambapo palikuwa na mgodi wa zamani wa dhahabu wa Barrick

Leave A Reply