Rais Samia Aipongeza Marekani Mbele Ya Kamala Harris – “Serikali Yenu Ina Maana Sana Kwetu”-Video
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpokea Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani Ikulu jijini Dar es Salaam na kuzungumza na vyombo vya habari leo Machi 30, 2023
KAMALA HARRIS: Marekani inaunga mkono kikamilifu ajenda ya Tanzania ya mageuzi ya kidemokrasia na ina dhamira thabiti ya kusaidia kuendeleza maadili ya kidemokrasia ya Tanzania.
Ziara ya Makamu wa Rais nchini Tanzania inathibitisha ubia huu imara baina ya nchi zetu mbili na itaimarisha zaidi ushirikiano katika biashara, jitihada za kutafuta ufumbuzi kuhusu usalama na uhakika wa chakula, ulinzi wa bayoanuai za majini, uwekezaji kwa wanawake na vijana, afya na kuimarisha demokrasia.
Katika kusaidia kuongeza wigo na kina cha uhusiano wetu rasmi, Serikali ya Marekani inakusudia kutoa Dola za Kimarekani milioni 560 kama msaada rasmi kwa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2024.
Hati ya Makubaliano itakayosainiwa kati ya Benki ya EXIM ya Marekani na Serikali ya Tanzania itapanua ushirikiano wa Kibiashara baina ya Marekani na Tanzania kwa kuziwezesha Kampuni za Kimarekani kuleta Nchini Tanzania bidhaa na Huduma bora za kibunifu
Makubaliano haya yatawezesha upatikanaji wa hadi Dola za Kimarekani milioni 500 kugharamia upelekaji wa Huduma na bidhaa katika sekta mbalimbali hususan, Miundombinu, Usafirishaji, Teknolojia ya Kidigitali, Nishati na Miradi ya Nishati jadidifu
Kuhusu Uendeshaji na Biashara ya Bandari, Marekani inalenga kusaidia jitihada za Serikali ya Tanzania kutumia kikamilifu fursa za uwekezaji na kuvutia wawekezaji wa aina mbalimbali, kulinda uwekezaji wake wa Kifedha na kuimarisha udhibiti wake wa Miundombinu hii muhimu kama Nchi huru