The House of Favourite Newspapers

Kamanda wa Polisi Arusha Apata Ajali

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amepata ajali katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya gari alilokuwa akilitumia kusafiria kupasuka gurudumu ‘tairi’ ya nyuma na kupoteza uelekeo.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Feb 26, 2018 na kusema gari hilo lililokuwa na watu watatu akiwemo msaidizi wakamanda na dereva, lilipata ajali baada ya kupasuka taili ya nyuma na kupoteza mwelekeo.

 

Mkumbo alipata maumivu kichwani lakini hali zao wote zinaendelea vizuri na wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Mount Meru.

Mambosasa Amemtaja Mwanamke Anayehusika Kifo cha Kada wa Chadema

Comments are closed.