The House of Favourite Newspapers

KAMATI YA BUNGE YAMKAANGA MKURUGENZI IGUNGA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesebu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeshindwa kuendelea na mahojiano na viongozi wa Halmashauri ya Igunga, mkoani Tabora kwa kushindwa kutekeleza maagizo mbalimbali ya kamati yaliyotolewa katika vikao vilivyopita ambapo halmashauri hiyo imerejea tena mbele ya kamati hiyo bila majibu ya maagizo yaliyotolewa na kamati.

 

Kamati hiyo imesema haijaridhshwa na utenda kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Revocatus Kuuli, na kwamba kamati imebaini kuwa mkurugenzi huyo mara nyingi hakai ofsini kwake na kuachia watu wengine majukumu yake jambo ambalo linapelekea shughuli mbalimbali za halmashauri kuyumba.

 

Halmashauri hiyo inadaiwa kushindwa kutekeleza maagizo ya kamati yaliyotolewa awali pamoja na yale yaliyolewa wakati kamati hiyo ikiwa imefanya ziara katika halmashauri hiyo.

 

Dakika chache mara baada ya viongozi wa halmashauri hiyo wakiongozwa na Mkurungenzi wao, Kuuli kuwasili mbele ya kamati kwaajili ya mahojiano, mwenyekiti wa kamati hiyo Vedasto Ngumbele Mwiru akamuulu viongozi wa halmashauri hiyo kuondoka kwakuwa wameshindwa kutekeleza maagizo yaliyolewa na kamati baada ya kubaini mapungufu mbalimbali ya kiutendaji.

Comments are closed.