The House of Favourite Newspapers

Kamati Ya Siasa CCM Kibiti Yakangua Miradi Ya Maendeleo, Yaridhika Na Utekelezaji Wa Ilani Ya Chama

0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti Juma Ndaruke akiongoza wajumbe wa Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.

Kibiti Pwani 8 Oktoba 2023: Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Juma Ndaruke leo Jumapili imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo na kusema kuwa imeridhika na utekelezaji wa ilani ya chama na kuipongeza Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mama Samia Salum kwa kupeleka fedha za miradi wilayani humo hali ambayo inazidi kuchochea ukuaji wa wilaya ya Kibiti.

Miradi ya maendeleo ambayo Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM imakagua ni pamoja na shule za msingi za Itonga na Jaribu ambazo kila moja ina madarasa 9 pamoja na majengo ya Utawala na yanametengewa bajeti ya kiasi cha Tzs 306 milioni kwa kila shule.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti Juma Ndaruke akizungumza na wajumbe wa Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya wakati wakifanya tathmini ya kutembelea miradi ya maendeleo wilayani humo ambapo kamati hiyo imesema imeridhika na utekelezaji wa ilani ya chama na kuwataka watumishi wa serikali kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa pesa zilizokusudiwa.

Mradi mwingine ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibiti ambayo ujenzi wake umengewanyika kwenye maeneo manne ambayo ni jingo la upasuaji ambalo limetengewa bajeti ya kiasi cha Tzs 237 millioni, Wodi ya wanawake kwa bajeti ya Tzs 235 milioni, Wodi ya wanaume kwa bajeti ya 235 milioni na Jengo la kuhifadhia maiti (Mortuary) kwa bajeti ya Tzs 93 milioni.

Mradi mwingine ambayo kamati hiyo ya siasa ilitembelea na kukagua ni kituo cha afya cha Nyamatanga ambacho kinajengwa kwa gharama ya Tzs 500 milioni pamoja na daraja la Mbwera lenye thamani ya 999 milioni.

Akizungumza kwenye kikao cha ndani cha kufanyia tathimini ya hali ya ujenzi wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibiti ambaye pia ndio mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Juma Ndaruke alisema kuwa chama kimeridhika na utekelezaji wa ilani na kuwapongeza wote wanaosimamia ujenzi wa miradi hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti Juma Ndaruke akihutubia na wajumbe wa Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya wakati wakifanya tathmini ya kutembelea miradi ya maendeleo wilayani humo ambapo kamati hiyo imesema imeridhika na utekelezaji wa ilani ya chama na kuwataka watumishi wa serikali kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa pesa zilizokusudiwa.

‘Nachukua fursa hii kumpongeza Rais na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama chetu Mama Samia Suluhu kwa kutenga bajeti ya utekelezaji wa miradi hii ambayo hivi punde tumemaliza kukagua. Miradi hii italeta uchochezi wa maendeleo kwenye wilaya yetu ya Kibiti. Kwa niaba ya Chama ngazi ya wilaya tunampongeza sana na sisi tunaahidi kuendelea kusimamia miradi hii kwa niaba ya wananchi wote wa wilaya ya Kibiti’, Ndaruke alisema.

Nawapongeza sana uongozi wa wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuweza kusimamia ujenzi wa miradi hii. Hata hivyo, kwa niaba ya chama nawaomba watumishi wote wa serikali ambao wanasimamia miradi hii kuhakikisha ya kwamba inakamilika kwa wakati na na pesa zilizokususudiwa, Ndaruke aliongeza.

Leave A Reply