Dakika 120 za Mazoezi Yanga Zatikisa Morogoro

KIKOSI cha timu ya Yanga kimewasili mkoani Morogoro juzi tayari kwa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ambapo kimejichimbia kwenye Chuo cha Bibilia maeneo ya Bigwa huku kukiwa na ulinzi mkali.

 

Kikosi cha Yanga kipo mkoani Morogoro tayari kwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara katika msimu wa 2019/20 huku kikiwa kimesajili majembe mapya kadhaa.

 

Aidha, wachezaji wote wa Yanga msimu huu ni pamoja na Cleofas Sospeter, Kelvin Yondani, Feisal Salum, Mohamed Issa ‘Banka’, Juma Mahadhi, Juma Abdul, Klaus Kindoki, Papy Kabamba Tshishimbi, Paul Godfrey, Andrew Vicent ‘Dante’, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Sadney Urikhob, Lamine Moro, Maybin Kalengo, Ali Hamad, Balama Mapinduzi.

Wengine ni Mustafa Suleiman, Gustafa Simon, Juma Balinya, Mrisho Ngassa, Ally Mtoni, Metacha Mnata, Muharami Salum, Farouk Shikhalo, Deus Kaseke, Raphael Daud, Abdulaziz Makame, Juma Abdul na Erick Msagati.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amefunguka kuwa, kikosi hicho kimeweka kambi eneo la Bigwa kutokana na kuona kuna usalama zaidi kutokana na utulivu ulivyo.

 

“Kikosi kimeshaelekea Morogoro kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu, kikosi kimefikia maeneo ya Bigwa kwa Masista na kitakaa hapo hadi msimu utakapoanza.

“Kocha Mwinyi Zahera atajiunga na kikosi baada ya mapumziko mafupi baada ya kumaliza michuano ya Afcon, tunaamini kikosi kitakuwa bora zaidi,” alisema Mwakalebela.

 

Hata hivyo, chanzo cha ndani kimesema kuwa kambi hiyo imewekwa ulinzi mkali sana na hakuna anayeruhusiwa kuzungumza na wachezaji au viongozi wa benchi la ufundi kama hatambuliki.

VIKOSI Vitatu vya Simba Hivi Hapa kwa Mifumo Yote


Loading...

Toa comment