Kigogo wa TRA, Miss Tanzania Waswekwa Tena Rumande

1-4-768x432

LEO April 1, 2016 Serikali iliwapandisha kizimbani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ Harry Kitilya, mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996 ambaye pia alikuwa Afisa Mwandamizi wa Benki ya Stanibic, Tawi la Tanzania, Bi. Shose Sinare pamoja na Sioi Solomoni kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja, kughushi nyaraka na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

 

Kesi hiyo ilipangwa kuendelea tena leo April 22, 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo imeahirishwa na Hakimu Mkazi Emillius Mchauru kwa sababu hakimu hajakamilisha uandikaji wa uamuzi wa kuondoa shitaka la utakatishaji fedha linalowakabili washtakiwa wote watatu.

Hakimu Emillius Mchauru ameipanga kesi hiyo kuendelea kusikilizwa tena April 27, 2016 ambapo watuhumiwa wote watatu wamerudishwa rumande mpaka siku ya kusikiliza kesi hiyo.

Takukuru iliwafikisha vigogo hao katika  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuwashtaki kwa makosa nane, ikiwemo tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, mwezi Machi mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda serikalini.


Toa comment