Kamishina wa Aridhi Kanda ya Dar es Salaam Bw. Idrisa Kayera amesimamisha zoezi la umilikishwaji wa viwanja vya makazi vilivyopo katika bonde la moringa kitalu 12 Kata ya Kibada Wilaya ya Kigamboni.
Kayera amesimamisha zoezi hilo baada ya kutembelea viwaja hivyo vilivyopo mtaa wa Moringa Wilaya ya Kigamboni na kugundua kuwa eneo hilo lina asili ya bonde na linalengwa na mikondo ya maji inayotoka maeneo mbalimbali ya mitaa hiyo.
Awali Viwanja hivyo vilitakiwa kupimwa na kumilikishwa kwa wakazi wa wilaya hiyo, lakini sasa eneo hilo litabadilishwa matumizi na litatumika kwa kilimo cha mjini yaani (Auburn farming)
Kayera amewaomba wakazi wa maeneo hayo kuwa wavumilivu wakati ambao Serikali inaandaa utaratibu mpya wa leseni ili kuwa kodishia wananchi watakaohitaji kufanya shughuli za kilimo Cha mjini katika Viwanja hivyo.