The House of Favourite Newspapers

KAMPENI: MTULIA AITEKA MAGOMENI KAGERA         

Mgombea Ubunge katika Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akinadi sera zake kwa wananchi wa Magomeni Kagera.
Mkutano  ukiendelea.

Baadhi ya mawaziri waliohudhuria mkutano huo.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ( katikati) akifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika mkutano huo.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia sera zake.

ZIKIWA zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia ameiteka Magomeni Kagera baada ya wakazi wa eneo hilo kufurika kwa wingi kusikiliza sera zake ambapo amewambia wakazi hao wampe kura ili aweze kuwatumikia vyema na  awaondolea  changamoto zilizopo  ndani ya jimbo hilo.

 

Hayo ameyaeleza leo wakati akiwa katika kampeni zake kwenye Viwanja vya Nyasi vilivyopo Magomeni ambapo alikuwa akinadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwaomba wananhi wa jimbo hilo kumpa kura.

Amesema kuwa aliacha Ubunge ili ajiunge na chama cha ushindi, chama chenye malengo, chama kinacholeta maendeleo kwa wananchi.
NA DENIS MTIMA/GPL

 

Comments are closed.