The House of Favourite Newspapers

AIRTEL YAWAZAWADIA WASHINDI WA SHINDA NA SMATIKA

Meneja mradi wa Airtel. Jane Matinde (kulia) akimkabidhi zawadi ya Modem mshindi wa promosheni hiyo.
Mtoto wa mama Esha aitwae Arif Mshana, akizungumzia furaha yake.
Meneja mradi wa Airtel. Jane Matinde (kulia) akimkabidhi mshindi simu ya Huawei,  Isack John.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando,akimpigia simu mmoja wa washindi. 

 

KAMPUNI ya simu za mikononi ya Airtel Leo imeendesha Promosheni ya Shinda na Smatika kwa kuwazawadia wateja wake 1,000 kwa siku bando lenye ukubwa wa GB 1 na wengine wakishinda simu za Huawei na Modem za Maajabu.

 

Washindi hao wamepatikana leo ikiwa ni muendelezo  wa promosheni ya nne ambapo sasa wateja 10,000 wamejishindia GB moja kila mmoja.

 

Kwa wakazi wa jiji la  Dar es Salaam leo tayari wamekabidhiwa zawadi zao na wale wa mikoani wataanza kupatiwa kuanzia kesho.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo makao makuu ya kampuni hiyo,  Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, alisema promosheni hiyo imekuwa ikichezeshwa kwa njia ya wazi bila upendeleo huku ikisimamiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.

 

“Tunayo furaha leo kuwa na wateja wetu ambao wamejishindia modem na simu, promosheni yetu bado inaendelea hivyo wateja wetu waendelee kununua vifurushi ili waweze kunufaika na zawadi zetu. Modem ya Maajabu ina uwezo wa kukuunganisha na marafiki zako,”.

Kwa upande wake, Esha Nasiri ambaye alijishindia Modem ya Maajabu, alisema anafurahia kushinda zawadi hiyo kutoka Airtel huku akisema ameshinda kutokana na kununua mara kwa mara vifurushi vya Intaneti vya Airtel.

 

“Kazi yangu  ni mjasiriamali natokea Ubungo, naishukuru kampuni ya Airtel kwa zawadi hii kwani imenifanya niwe na fahari na nitaendelea kutumia mtandao huu.

 

“Binafsi sina matumizi ya Intaneti,  hivyo nitampatia mwanangu ambaye hutumia kwenye kompyuta yake wakati akijisomea masomo yake kwa njia ya Tehama,” alisema Esha.

 

Naye mtoto wa Esha aitwaye Arif Mshana aliishukuru kampuni hiyo kwa kumzawadia mama yake Modem ya Maajabu kwani itamsaidia kuweza kujisomea mtandaoni.

 

 

 

Comments are closed.