The House of Favourite Newspapers

Kampeni ya binti thamani kurindima Dar

0

Walioko mbele kutoka kushoto ni, Meneja Mipango wa Don Bosco, Rosemary Tery, Mkuu wa Chuo cha Don Bosco Mkoa wa Dar es Salaam, Jose Kaiphan na Mratibu, Agnes Mgongo.

Baadhi ya wasichana watakaoshiriki kampeni hiyo wakiwa kwenye mkutano huo na wanahabari.

Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.

KAMPENI ya Binti Thamani inayoratibiwa na Taasisi ya Don Bosco Neti kwa kushirikiana na Kampuni ya Trumark, kesho itaendesha kampeni yake ijulikanayo ‘Binti Thamani’ yenye lengo la kuibua na kutatua changamoto za uelewa kwa vijana hasa wa kike kujua na kutambua fursa za kujiendeleza na kufanikiwa kupitia mafunzo ya ufundi baada ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa kampeni hiyo, Agnes Mgongo amesema kuwa Don Bosco Neti hufanya kazi zake katika nchi zaidi ya 132 duniani lengo likiwa ni kuboresha na kufanikisha maisha ya vijana hasa wa kike ili kuwaweza kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha wasichana wengi wanapenda mafunzo ya ufundi stadi.

Mgongo amesema Don Bosco imekuwa ikitoa mafunzo ya ufundi stadi kama uchoraji, useremala na ufundi umeme wa viwandani kwa vijana wa Kitanzania kupitia vyuo vyao vya ufundi vilivyopo Dar es Salaam, Iringa na Dodoma huku changamoto mbalimbali kwa wasichana zikiongezeka kwa kiasi kidogo.

Aidha, Mgongo alifafanua kuwa kampeni hiyo inatarajia kufanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kwa kuwakutanisha wasichana wapatao 1,000 wa shule za jijini Dar, pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wazazi na walimu ili kuhakikisha uhamasishaji unafanikiwa.

Hata hivyo, amesema kuwa Kampeni ya Binti Thamani imedhamiria kuhamasisha na kuleta mwamko mpya kwa vijana wa kike katika kushiriki mafunzo ya ufundi na kujikwamua kimaisha na kwamba wao ni taifa la kesho hasa linalotegemewa katika jamii.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kampeni hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kesho Novemba 17, kwenye Ukumbi wa King Solomon huku kwa Mkoa wa Dodoma ikihitimishwa Novemba 28, mwaka huu katika Chuo cha Ufundi cha Don Bosco kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 10 jioni huku mshereheshaji akiwa ni MC Pilipili msanii Elias Barnaba akitarajiwa kutoa burudani.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

 

Leave A Reply