The House of Favourite Newspapers

Kampeni Ya Cha Wote Yafikia Tamati Ikiwatunukia Mamilioni Zaidi Ya Wateja 28,600

0
Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta (kushoto) akimpongeza mmoja wa washindi wa shilingi milioni moja, Devotha Gerald Kweka kwenye hafla ya kuwakabidhi pesa zao.

Kampeni ya ‘Cha Wote’ iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo kwa kuwazawadia zawadi mbalimbali wateja wake waliokuwa wakifanya miamala na kununua vifurushi vya intaneti na muda wa maongezi, leo imefikia tamati huku ikiwa imewatunukia mamilioni wateja wake zaidi ya 28,600.

Akizungumza kwenye kutamatisha kampeni hiyo, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta amesema;

Mmoja washindi wa shilingi milioni moja, Devotha Gerald Kweka, akishangilia na mfano wa hundi kwenye hafla ya kuwakabidhi pesa zao leo.

“Leo tumepata washindi wetu wa mwisho wa kampeni yetu ya Cha Wote ambapo kuna wawakilishi waliokuja hapa ofisini kwetu kupokea zawadi zao na wapo ambao tutawatumia kutokana na changamoto mbalimbali zilizowafanya washindwe kufika hapa leo.

“Mpaka sasa tumeshatoa zawadi kwa zaidi ya washindi 28,600 waliojishindia hadi shilingi milioni tano.

“Kwa hiyo kampeni yetu imeweza kugusa maisha ya Watanzania mbalimbali kwenye maeneo tofauti tofauti ikiwemo kwenye ada, mitaji, kulipia kodi za majengo na kuongeza furaha kwenye nyuso za wateja wetu wa Tigo Pesa.

“Kwa hiyo tunawaomba wateja wetu waendelee kufanya miamala ya Tigo Pesa kwani kuna zawadi kemkem zinakuja kuelekea kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya”.  Alimaliza kusema meneja huyo.

Leave A Reply