The House of Favourite Newspapers

Tigo Yamtangaza Mshindi Wa Funga Dimba La Kampeni Ya ‘Cha Wote’, Aondoka Na Milioni 5

0
Meneja wa Tigo kanda ya Ilala, Edwin Mgoa.

KAMPUNI ya Tigo kupitia shindano lao la Cha Wote leo imemtamngaza Kassim Mkono kuwa mshindi wa shilingi milioni 5 katika shindano la Chawote lililofikia tamati leo ambalo lilikuwa likiendeshwa na kampuni ya simu ya tigo.

Mshindi huyo ametangazwa  na Meneja wa Tigo kanda ya Ilala Edwin Mgoa ambapo amesema Kassim Mkono kutoka Buguruni Dar es Salaam amekuwa mshindi wa jumla wa shindano hilo ambalo lilidumu kwa muda wa miezi mitatu huku mshindi wa shindano hilo Kassim akisema fedha hizo ni mtaji mkubwa kwake.

Shindano hilo limefikia tamati baada ya kumtangaza mshindi wa mwisho wa shindo hilo Kassim Mkono Mlekwa aliyejishindia milioni 5.

Meneja wa Tigo kanda ya ilala Edwin Mgoa amesema Kassim Mkono Mlekwa ambaye ni mkazi wa Buguruni kwa madenge mkoani Dar es Salaam amekuwa mshindi wa jumla wa shindano hilo ambalo lilidumu kwa muda wa miezi mitatu.

Edwin Mgoa mesema wateja wa mtandao wa Tigo ambao wametumia Tigo pesa wamefanikiwa

Kushinda   zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslim pamoja muda wa maongezi, sms na bando za mtandao huo.

Mshindi wa shindano hilo Kassim Mlekwa alisema hakuamini alipopigiwa simu na kufikiri kwamba walikuwa ni matapeli walikuwa wakitaka  kumuibia.

Amewataka wateja wengine wa mtandao huo kucheza michezo mbalimbali ya bahati nasibu kwakuwa anaamini kwamba mshindi hua apangwi ila inatokea kama ilivyokuwa kwake.

Leave A Reply