Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu Bora za Miti na Vipando wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), SACC Caroline Malundo, akiwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Green Village Estate, Bwana Reeves Ngalemwa akimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, CC Prof. Dos Santos Silayo,wamehitimisha kilele cha kampeni ya upandaji miti 1000 iliyokuwa na malengo ya kuhamasisha wakazi wa Green Village na maeneo jirani umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa njia ya upandaji miti. Mti hiyo 1000 ilipatikana kwa ufadhili wa TFS Ofisi ya Kinondoni.