The House of Favourite Newspapers

Edosama kutoa madawati milioni 1.5 nchi nzima

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Ltd, Edward Maduhu (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu mradi wa kutengeneza madawati hayo na changamoto ya kukwamishwa kwa mradi huo na baadhi ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na watendaji wa serikali. Kulia ni Meneja Mwendeshaji wa Shule za St Marys, Didas Mhoja  na kushoto ni  mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Jonas Mnzava.
 Maduhu akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam  jana, madawati ambayo kampuni hiyo itayatoa kusaidia jitihada za Rais Dk. John Magufuli za kusaidia elimu bure nchini.
 Wanahabari wakichukua taarifa katika hafla hiyo.
 Mkutano ukiendelea.
 Didas Mhoja (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mjasiriamali na mtaalamu wa mazao ya misitu kutoka shamba la miti la Sao Hill Mafinga mkoani Iringa, Oscar Kaduma akizungumza katika mkutano huo.
   Edward Maduhu, akiwa amesimama juu ya ubao wanaotengenezea madawati hayo kuonyesha uimara wake.
 Hapa akionesha magamba ya miti yanayotengenezea  samani hizo.
 Hapa akionesha meza iliyotengenezwa kwa mabaki ya mbao.
Mkurugenzi Maduhu akionesha dirisha lililotengenezwa kwa mabaki ya mbao.
Na Dotto Mwaibale

 KAMPUNI ya Edosama Hardware Ltd imesema kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Magufuli za kutoa elimu bure kampuni hiyo imeahidi kutoa madawati milioni moja na nusu kwa nchi nzima.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Edward Maduhu wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu mradi wa kutengeneza madawati hayo na changamoto ya kukwamishwa kwa mradi huo na baadhi ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na watendaji wa serikali.

Alisema madawati hayo yanatokana na mradi uliobuniwa na kampuni hiyo ambapo awali walifanya utafiti wa miaka mitano ambao ulitumia zaidi ya sh.bilioni 1.2.

“Pamoja na jitihada zetu za kutaka kupunguza uhaba wa madawati kama siyo kumaliza kabisa changamoto hii hapa nchini kwa kuishirikisha serikali katika jambo hili ikiwa ni pamoja na kukaa nayo vikao mbalimbali, hakuna majibu yoyote tuliyopata,” alisema Maduhu.

Maduhu alisema wakati Rais Dk.John Magufuli akizungumza na wafanyabiashara alisema kama kutakuwa na mfanyabiashara anataka kufanya uwekezaji lakini anakwamishwa na mtendaji wa serikali ambaye yupo katika uteuzi wake ni vizuri akapewa taarifa ili achukuliwe hatua.

Alisema mradi huo una tija kubwa kwa taifa na utasaidia sana katika kutekeleza agizo la rais la kutoa elimu bure ingawa sasa ni miaka miwili imepita bila kupatiwa majibu na unakwamishwa na mtandao wa watendaji wa serikali wakishirikiana na wafanyabiashara wakubwa wa madawati.

“Kama kweli serikali na viongozi wake wana nia ya dhati na ya kweli ya kumaliza changamoto hii ya madawati nchini kwa nini inaukwepa mradi huu wa madawati ya bure ambao utaokoa fedha za umma zaidi ya sh. bilioni 150 lakini hadi leo hii ni miaka miwili serikali imekaa kimya lakini wakati huohuo inaendelea kununua madawati kwa bei kubwa na yasiyo na ubora na kuacha madawati imara yenye garantii ya miaka mitano?” alihoji Maduhu.

Maduhu aliongeza kuwa ndoto ya kampuni hiyo ni kuwasaidia wanafunzi zaidi ya 4,500,000 wanaohitaji madawati nchini na pia kutoa ajira kwa Watanzania 100,000 lakini ndoto hiyo inaweza kutimia iwapo serikali itaona kuwa wanachokisema kinawezekana kama itakutana na watendaji wa kampuni hiyo kuwapa taarifa za kina kuhusu mpango wao huo wa madawati bure.

Leave A Reply