The House of Favourite Newspapers

Kampuni Ya Mafuta Ya PUMA Ilivyotoa Zawadi Kwa Watoa Huduma Bora, Yaahidi Makubwa

0
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeendeleza utaratibu wa kuwatambua na kuwazawadia watoa huduma bora huku ikiahidi kuendelea kusimama imara kuendeleza rekodi ya kuwa kampuni namba moja ya mafuta nchini.

Aidha, serikali imeridhishwa na mwenendo wa kampuni hiyo katika utoajia wa huduma za  mafuta, gesi na vilainishi na kuahidi kuendelea kuwa nayo bega kwa bega.

Mwakilishi wa Kituo cha Mafuta cha Puma Arusha, akikabidhiwa tuzo na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, baada ya kituo hicho kuibuka mshindi wa kwanza. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy hapa nchini, Fatma Abdallah. 

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo, kuwatambua, kuwatangaza na kuwapa zawadi waendeshaji bora wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini, iliyofanyika, Oktoba 20, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Fatma Abdallah amesema mafanikio makubwa inayoyapata Puma yanatokana weledi, kujituma na uwajibikaji unaofanyika vituoni.

Amesema watoa huduma hao wamekuwa wakiwapatia wateja wao huduma iliyobora kila wanapotembelea vituoni, hivyo watoa huduma hao ndiyo jicho la kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Fatma, lengo la kampuni hiyo ni kuwapa huduma bora Watanzania kufikia malengo yao katika maisha hivyo wataendelea kuboresha huduma kulingana na wakati na mahitaji.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, amesema serikali imeridhishwa na mwenendo wa kampuni hiyo katika utoaji wa huduma za mafuta, gesi na vilainishi na kuahidi kuendelea kuwa nayo bega kwa bega.

Aibu Waziri Judith ameipongeza kampuni hiyo kwa ubunifu mbalimbali inaoufanya ikiwemo  kuwatambua na kutoa zawadi kwa waendeshaji bora wa vituo vya mafuta vilivyo chini ya kampuni hiyo nchi nzima ambao wanafanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali ya utoaji wa huduma na bidhaa za Puma Energy.

Amesema huduma bora ndizo zinazoifanya kampuni hiyo iendelee kuwa namba moja kwa utoaji wa huduma za mafuta nchini, hivyo itaendelea kuiunga mkono kuhakikisha inaendelea kuwa katika ubora unaitakiwa na kuiletea nchi mapato zaidi.

Naibu Waziri Judith amesema kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Puma Energy Tanzani ni kiongozi wa soko katika usambazaji na uuzaji wa bidhaa za mafuta ya petrol nchini.

Amesema lengo la kampuni hiyo ni kuwapa huduma bora Watanzania kufikia malengo yao katika maisha hivyo wataendelea kuboresha huduma kulingana na wakati na mahitaji.

Katika tuzo hizo Kituo cha Mafuta cha Puma Arusha kiliibuka mshindi wa kwanza huku Puma Upanga ikitwaa nafasi pili kwa huduma bora.

Leave A Reply