The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya T-PESA: Maadhimisho Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa Umeleta Chachu Katika Utoaji Elimu kwa Wateja

0
Bw. Thomas Lemunge Afisa Mauzo Shirika la Mawasiliano Tanzania akitoa elimu kuhusu huduma za T- PESA kwa kwa wakazi wa Arusha walipotembelea Banda la T-PESA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanayoendelea katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.

KAMPUNI Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, T-PESA imesema kuwa uwepo wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa umeleta chachu katika utoaji wa elimu kwa Wateja wake na Wananchi kwa ujumla kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo.

Hayo yameelezwa na Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayofanyika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.

Amesema Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha Taasisi ndogo za fedha, Mabenki, Mifuko ya Hifadhi za Jamii pamoja na wajasiriamali yameisaidia Kampuni ya T-PESA kukutana na Wananchi na kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha mtandao na fursa mbalimbali zinazopatikana katika Kampuni hiyo zinazoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Bi. Catherine Simba wa Shirika la Mawasiliano Tanzania akitoa elimu kuhusu huduma za T- PESA kwa mkazi wa Arusha alipotembelea Banda la T-PESA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanayoendelea katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.

Amesema katika kuunga juhudi za Serikali za kutatua changamoto ya ajira kwa vijana T-PESA imetoa fursa mbalimbali kwa vijana zinazoweza kuwasaidia kujitengenezea kipato na hivyo kujikwamua kiuchumi.

“T-PESA inazo fursa mbalimbali hasa kwa vijana ikiwa ni pamoja na uwakala ambapo wanaweza kufanya biashara hii ya kuwa Wakala na kujipatia kipato cha kusaidia familia zao kwani T-PESA tunatoa kamisheni kubwa zaidi ukilinganisha na mitandao mingine,” amesema Bi. Adeline.

Bw. Thomas Lemunge Afisa Mauzo Shirika la Mawasiliano Tanzania akitoa elimu kuhusu huduma za T- PESA kwa kwa wakazi wa Arusha walipotembelea Banda la T-PESA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanayoendelea katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.

Aidha amesema Maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine yametoa fursa kwa Kampuni hiyo kukutana na Wateja na Wananchi kwa ukubwa zaidi na kujibu hoja, maswali na kero zao na hivyo maadhimisho hayo yamekuwa muhimu katika kupata mrejesho sahihi kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na T-PESA.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanafanyika kwa mara ya tatu sasa huku kwa mwaka huu yakibeba kaulimbiu ya, ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi na kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

Leave A Reply