Kampuni ya UDA yakanusha kufilisika
- UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka mabasi 7 makukuu na mabovu Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka 2015 yakiwemo mabasi 255 ya kawaida na mabasi makubwa – Hercalus, mapya na ya kisasa kabisa duniani (ya BRT) 140.
- Ndani ya miaka 3, kampuni ya UDA imekuwa kwa zaidi ya asilimia 5,000
- Kampuni hii imeweza kufanya maandalizi yote ya kuwezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi mkubwa. Mbali na kununua mabasi, kampuni imeweze kununua mtambo bora na wa kisasa kabisa duniani wa kukusanya nauli na kuongezea mabasi (Intelligent Transportation System – ITS) wenye thamani kubwa kutoka Ubelgiji na Ujerumani. Vile vile kampuni imeweza kusaili na kufundisha madereva wa Kitanzania zaidi ya 300 na kuwaajiri kwa ajiri ya kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project)
- Kampuni imejenga karakana bora na imara na kununua vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya mabasi yake ya kawaida na mwendo haraka.
- Kampuni imepeleka watendaji wake kwenye miradi mbalimbali ya BRT duniani ili kupata uzoefu wa kuwawezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi. Vile vile Kampuni imeweza kuajiri wataalam kutoka nje (expatriates) kwa ajiri kuongezea nguvu wataalam wake wa ndani.
Imetolewa na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED