The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya Vifaa vya Umeme wa Jua D.light Tanzania Yafungua Kituo Dar

0
Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora (katikati) akikata utepe kuzindua kituo cha huduma kwa wateja na mauzo cha vifaa vya umeme wa jua vya d.light Makumbusho jijini Dar Es Salaam. Wengine kulia ni Mkurugeni wa d.light Tanzania, Charles Natai na kushoto ni Meneja Biashara d.light kanda ya Pwani , Gasper Mrosso.

 

 

 

Afisa Mauzo mkoa wa Dar Es Salaam, Mosenye Chacha akitoa maelezo kwa Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora jinsi vifaa vya umeme wa jua d.light vinavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho kilichopo Makumbusho jijini Dar Es Salaam.

 

 

 

Mkurugeni wa Dlight Tanzania, Charles Natai (kushoto) akimkabidhi Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora zawadi ya kifaa kinachotumia umeme wa jua kutoka d.Light Tanzania, Kifaa hichi kinatoa mwanga , kina radio na kina sehemu ya USB kwa ajili ya kuchajia simu, mara baada ya uzinduzi wa kituo hichi kilichopo Makumbusho jijini Dar Es Salaam.

 

 

 

Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja na mauzo cha vifaa vya umeme wa jua d.light Makumbusho jijini Dar Es Salaam.Wengine kushoto ni Mkurugeni wa d.light Tanzania, Charles Natai na Meneja Biashara d.light kanda ya Pwani , Gasper Mrosso.

 

 

 

Mteja wa d.light, Frank Mchaki akielezea namna vifaa vya umeme wa jua vya d.light vinavyofanya kazi.

 

 

 

Fundi wa vifaa vya umeme wa jua vya d.light, Idd Ramadhani (kulia) akitoa maelezo kwa Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora namna wanavyojali na kutoa huduma ya ufundi kwa wateja wao mara baada ya kununua vifaa hivyo.
Leave A Reply