The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya Vivo Energy Yawakumbuka Wanafunzi Wenye Uhitaji Sekondari Ya Jangwani

0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mwasiliano wa Vivo Energy, Grace Kijo (kulia) akizungumza na wanafunzi kwenye hafla hiyo.

Dar es Salaam, 1 Desemba 2023: Kampuni ya mafuta ya Vivo Energy inayomiliki vituo vya mafuta vya Engen, leo imefanya matendo ya huruma kwa kuwapelekea wanafunzi wa Sekondari ya Jangwani misaada mbalimbali kama vile taulo za kike, fimbo za kutembelea na mahitaji mengine muhimu kwao.

Alizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania, Mohamed Bougriba amesema wameamua kupeleka msaada huo kwa wanafunzi hao wenye changamoto kwa ajili ya kusaidia kutimiza ndoto.

“Katika kushirikiana na jamii tumeonelea turudishe tunachokipata kwa jamii kwa kuwakumbuka wanafunzi hawa ili tuwasaidie kutimiza ndoto zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania, Mohamed Bougriba akimkabidhi mmoja wa wanafunzi sehemu ya msaada huo kwa niaba ya wenzake. Kushoto ni Makamu Mkuu wa shule hiyo Paulina Aweda.

Kwa upande Makamu Mkuu wa shule hiyo, Paulina Aweda ameishukuru Vivo Energy kwa kuikumbuka shule hiyo inayopokea watoto wenye ulemavu ambao wengi wanaishi shuleni hapo lakini wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa vitu mbalimbali hiyo msaada huo umelenga sehemu sahihi kabisa.

Afisa Elimu Kata ya Upanga, Imaculata Ngure akizungumza na vyombo vya habari baada ya kushuhudia tukio la kupokea msaada huo. 

Mwalimu Aweda amesema shule hiyo inayofundisha wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita inawanafunzi wenye uhitaji maalumi (ulemavu) zaidi ya mia moja hivyo msaada huo utakwenda kuwapunguzia changamoto walizokuwa nazo na kuwafanya wasome vizuri na hivyo kufaulu vizuri na kutimiza ndoto zao.

Baada ya Vivo Energy kukabidhi msaada huo.

Kwa niaba ya shule hii nawapongeza sana Vivo Energy na nawaombea kwa Mungu kampuni yao izidi kubarikiwa na napenda kutumia nafasi hii kuwakaribisha wadau wengine wenye moyo wa huruma kuwakumbuka wanafunzi hawa.

Naye Afisa Elimu Kata ya Upanga, Imaculata Ngure ameipongeza Vivo Energy kwa msaada huo ambao unaokwenda kuwafanya wanafunzi hao kupunguziwa changamoto ambazo huenda zingine zilikuwa zikiwafanya washindwe kusoma vizuri. HABARI/PICHA : RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply