The House of Favourite Newspapers

Kampuni za Jumia, Tecno Kuuza Bidhaa Kwa Mtandao

0
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za TECNO, Eric Mkomoye (kulia) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.
Meneja Jumia Tanzania nchini, Hilda Kinyunyu (Kulia) akifafanua jambo.

KAMPUNI ya Jumia Tanzania inayouza bidhaa kwa njia ya mtandao, itashirikiana na kampuni za simu za Tigo na Tecno kuuza bidhaa zake kwa bei nafuu jambo litakalowazesha Watanzania wa vipato mbalimbali kuagiza na kupata bidhaa hizo kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano wa TECNO, Eric Mkomoye, amesema kampuni yake na Jumia Tanzania wameamua kuungana kutoa huduma popote mteja alipo kwa njia ya mtandao.
”Kutakuwa na Jumia Mobile Week itakayoanza Mei 22 -28 mwaka huu ikiwa maalumu kwa ajili ya mauzo ya simu na vifaa vyake kutoka makampuni makubwa Tanzania yanayoshirikiana na Jumia. Kutakuwa na  punguzo kubwa na zawadi mbalimbali kwa wateja watakaonunua bidhaa hizo katika website yao ,” alisema Mkomoye.

Naye meneja wa kampuni hiyo nchini, Hilda Kinyunyu, alisema
wateja wao wanaweza kuagiza simu kupitia mtandao wa Jumia na kuchagua bidhaa wanazotaka kisha wanajaza taarifa zao za msingi kama namba za simu na eneo wanalotaka bidhaa waletewe na watafikishiwa,

Malipo yatafanyika baada ya mteja kupata bidhaa husika na  kuridhika nayo,” alieleza Kinyunyu .
Aliendelea kufafanua kuwa kampuni ya Tecno Mobile itakuwa na duka maalum katika mtandao wa Jumia ambapo simu za kampuni hiyo ikiwemo simu mpya maarufu ya Tecno Camon CX itapatikana. Pia Tecno Phantom 6, W5 na l9 plus zitapatikana. Mteja atakayweka oda ya simu za Tecno Mobile katika mtandao wa Jumia atapata zawadi mbalimbali zitakazomfikia pamoja na simu hiyo.
“Kampuni yetu inauza bidhaa zake kwa bei nafuu zaidi katika masoko ya mitandaoni kuliko mtandao wowote nchini Tanzania na bidhaa mbalimbali zinapatikana  kuanzia zinazohusu fasheni, vifaa vya umeme, viatu, saa, michezo ya kubahatisha , simu za mkononi, Laptops na kompyuta, vipodozi na samani.

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply