The House of Favourite Newspapers

Kamusoko amtia hasira Chuji

0

Wilbert Molandi,

Dar es Salaam

KIUNGO wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’ amesema anapatwa na hasira pale uwezo wake unapofananishwa na kiungo Thabani Kamusoko na sasa anapambana kurejesha makali yake ya zamani.

Chuji aliondoka Yanga msimu wa Ligi Kuu Bara 2013/2014 baada ya mkataba wake kumalizika na sasa anachezea Mwadui FC ya Shinyanga inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Kamusoko ni kiungo raia wa Zimbabwe anayeichezea Yanga, kutokana na uwezo wake mashabiki wamekuwa wakimfananisha na Chuji kiuchezaji wakati mwingine ikielezwa ana uwezo zaidi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Chuji alisema anaheshimu uwezo wa Kamusoko na hiyo ni changamoto kwake kuhakikisha anarejesha kiwango chake.

Chuji anayesifika kwa uwezo wake wa kupiga pasi fupi na ndefu alisema, anaamini majeraha ya enka na kidole tangu akiwa Yanga na sasa Mwadui, ndiyo yaliyofifisha uwezo wake.

“Siku zote ukiona watu wanakuzungumzia au kukufafanisha na mchezaji profesheno mwenye kiwango kikubwa, basi ujue wanakubali kiwango chako, ndivyo ilivyo kwangu na kwa Kamusoko.

“Majeraha ya kidole na enka yaliniweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, ndiyo kwanza nimerejea mazoezini sasa najipanga kurejea kwenye uwezo wangu na Kamusoko amekuwa chachu kwangu,” alisema Chuji.

 

Leave A Reply