Kamusoko Ndiyo Kwanza Kaanza Upya

Thaban Kamusoko raia wa Zimbabwe akifanya mazoezi.

KIUNGO wa Kimataifa wa Yanga, Thaban Kamusoko raia wa Zimbabwe ameonekana bado kutokuwa fiti kutokana na kuongezewa muda zaidi wa kuendelea na matibabu.

 

Kamusoko aliumia goti mwishoni mwa mwaka jana ambapo kikombe cha goti kilipasuka katika mguu wa kushoto hali iliyosababisha kukaa nje hadi sasa.

 

“Kamusoko bado hayupo vizuri anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Randan iliyopo Posta ambayo ni mahususi kwa ajili ya miguu.

 

“Daktari amemuongezea wiki tatu mbele za kuendelea kujiangalia kutokana na bado kutokuwa fiti katika suala zima la kukimbia kwa kuwa aliumia ‘ligamenti’ za kwenye goti, hivyo atakapokaa sawa atarejea uwanjani,” alisema Ten ambaye mashabiki wa Yanga wanamsifu kwa kuboresha matumizi ya teknolojia ya mitandao ya kijamii klabuni kwao. Kiungo huyo katika msimu huu amecheza mechi nne pekee za ligi kuu.

Loading...

Toa comment