The House of Favourite Newspapers

Kanali Doumbouya Amteua Beavogui Kuwa Waziri Mkuu

0

Kiongozi wa jeshi la Guinea amemtaja mfanyikazi wa zamani wa serikali Mohamed Beavogui kama waziri mkuu kusimamia mabadiliko ya utawala wa raia kufuatia mapinduzi ya mwezi uliopita.

 

Beavogui, 68, ni mtaalam wa fedha katika sekta ya kilimo. Ana uhusiano wa kifamilia na mwanadiplomasia wa zamani wa Guinea ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa kwanza wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika, ripoti za mashirika ya habari zinasema.

 

Uteuzi wake ulitangazwa Jumatano katika amri iliyosomwa kwenye runinga ya taifa. Kiongozi wa mapinduzi Kanali Mamady Doumbouya Ijumaa iliyopita aliapishwa kuwa rais wa mpito.

 

Amezuiwa kugombea uchaguzi wa baadaye chini ya mipango ya kurejesha utawala wa kiraia. Aliahidi kuandaa uchaguzi huru , wa kuaminika na wa uwazi lakini hakusema utafanyika lini.

Leave A Reply