The House of Favourite Newspapers

Tamisemi Yafafanua Wanafunzi Wanaotumia Mtumbwi Kwenda Shule

0

OFISI ya Rais TAMISEMI imekiri kuona video fupi inayosambaa kwenye mitandao ikionesha wanafunzi wakitumia mitumbwi kwenda na kutoka shuleni.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tamisemi wamesema; “TUMEGUSWA, Ofisi ya Rais Tamisemi imeona video fupi inayotembea kwenye mitandao ikionesha wanafunzi wakitumia mitumbwi kwenda au kutoka shuleni. Ni kweli kwamba bado tunachangamoto ya wanafunzi wanaoishi kwenye maeneo ya visiwa vilivyopo katika bahari na vile vya kwenye mito na maziwa.

 

Serikali imekuwa ikijenga mabweni kwenye maeneo haya ikiwemo Halmashauri za Kibiti, Mafia na Ukerewe ambazo zina shule zenye sifa hizi. Pia, OR TAMISEMI itaendelea kuhakikisha mazingira ya shule hizo yanaendelea kuboreshwa ili kulinda maisha ya wanafunzi na kuondoa vikwazo katika elimu yao.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply