The House of Favourite Newspapers

Kanali Mstaafu: Magufuli Kajitoa Kafara Tumuunge Mkono

0

1.Mhadhiri na Mtafiti katika masuala ya habari Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Ramadhani akitoa taarifa yake mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Mhadhiri na Mtafiti katika Masuala ya Habari, Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Ramadhani akitoa taarifa yake mbele ya wanahabari (hawapo pichani). 2.Wanahabari wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.

MHADHIRI na mtafiti katika masula ya habari ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Ramadhani amesema kuwa Rais Magufuli amejitoa kafara kwa ustawi na maendeleo ya nchi na wananchi wake kwa kuhitaji uadilifu, haki, usawa na heshima hivyo anapaswa kumuungwa mkono katika utendaji wake.

Hayo ameyasema leo alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam juu ya Magufuli anavyopaswa kuombewa kutokana na utendaji kazi wake wa kupambana na mafisadi.

Alifafanua kuwa wanaombeza na kunyong’onyesha jitihada za kiongozi huyo wasionewe aibu kwani ni wachache lakini ambao ni hatari kubwa kwa taifa linalohitaji amani, mshikamano na ustawi wa nchi yetu.

“Hivi ni vita vya ukombozi wa uchumi. Tunao maadui wa ndani na nje ambao hawatafurahia jitihada hizo anazochukua kiongozi wetu. Tusimame imara tusiyumbe wala kukubali kushindwa kwani siri ya mafanikio yetu ni umoja na mshikamano,” alisema.

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply