The House of Favourite Newspapers

Kangi Lugola Aibuka Zenji kwa Dkt. Shein

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,  yuko visiwani Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kikazi visiwani humo ambapo amekutana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein.

Waziri huyo amekutana na Rais wa Zanzibar, Dkt Shein leo Novemba 19 Ikulu  kwa nia ya kujitambulisha akiambatana na baadhi ya viongozi wake wa wizara.

 

Miongoni mwa viongozi walioambatana na Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,  na Naibu Katibu Mkuu, Kailima Ramadhani.

Hii ni mara ya kwanza kwake kuwasili visiwani humo tangu alipoteuliwa na Rais Magufuli kushika nafasi hiyo Julai 1 mwaka huu baada kuenguliwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kudhibiti ajali za barabarani.

Comments are closed.